

Kocha mkuu wa klabu ya Yanga, Mwinyi Zahera amesema tangu jana hajui alipo beki wa kikosi hicho Abdalah Haji Shaibu Ninja, imeelezwa.
Taarifa imeeleza Ninja alikatazwa kufanya mazoezi ya klabu hiyo kutokana na barua kutoka TFF ya kumsimamisha kucheza mechi za ligi kuu Tanzania Bara mpaka pale atakapohojiwa na Kamati ya Nidhamu.
Hatua hiyo ilikuja kutokana na kitendo cha kumpiga kiwiko mchezaji wa Coastal Union katika mchezo wa ligi uliomalizika kwa sare ya mabao 1-1.
Wakati Ninja akisubiri hukumu, mpaka sasa Zahera amesema hajamuona na hajajua kipi kimempata beki huyo ambaye amekuwa sehemu ya kikosi cha kwanza Yanga.
Yanga itakuwa na kibarua kesho katika mchezo wa ligi dhidi ya JKT Tanzania ambao utapigwa Uwanja wa CCM Mkwakwani Tanga.




0 Comments