

ALLY Bushiri kocha wa Mbao FC, amesema wamejiandaa kubeba pointi tatu leo mbele ya vinara wa ligi, Yanga utakaochezwa uwanja wa CCM Kirumba.
Bushiri amesema maandalizi yapo vizuri na wachezaji wana morali kubwa ya kupambana hivyo imani kubwa ni kubaki na pointi tatu nyumbani.
"Mzunguko wa kwanza tuliacha pointi zetu kwao hivyo nao ni zamu yao kuacha pointi nyumbani, kila kitu kinawezekana na hizo ndizo hesabu zetu kwa sasa.
"Nawaheshimu wapinzani wangu najua wana hasira baada ya kupoteza mchezo wao dhidi ya Simba ila wasitarajie kupata mpenyo kwangu nami nazihitaji pointi tatu," amesema Bushiri.




0 Comments