Windows

MTIBWA SUGAR WAPANIA KUIFUNGA MDOMO KMC LEO UGENINI


KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Zuber Katwila amesema atawafunga KMC kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara ili kuwaziba mdomo wale wanaoibeza timu yake kwenye mchezo utakaochezwa leo uwanja wa Uhuru.

Mtibwa Sugar kwenye michezo minne waliyocheza hivi karibuni wamepoteza michezo mitatu na kupata sare mchezo mmoja tofauti na wapinzani wao KMC ambao kwenye michezo minne walipata sare tatu na kupoteza mchezo mmoja.

Katwila amesema anatambua ugumu wa ligi ulivyo pamoja na matokeo mabovu anayopata hali ambayo imemfanya awape darasa wachezaji wake warejee kwenye ubora.

"Mpira wetu una changamoto nyingi na kila kitu kina wakati wake naona wapinzani wetu wanapiga kelele sasa ni muda wetu wa kurejea kwenye ubora na kufanya kile ambacho mashabiki wanakitarajia.

"Kupoteza michezo ni jambo ambalo linaigharimu timu na tatizo kubwa tulilonalo ni kwenye safu ya ushambuliaji kushindwa kumalizia nafasi ila bado tuna imani ya kupata matokeo," amesema Katwila.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza Mtibwa wakiwa wenyeji walikubali kugawana pointi moja baada ya kutoa sare ya kufungana bao 1-1 uwanja wa Manungu.


Post a Comment

0 Comments