BAADAA ya kushinda michezo mitatu bila kuruhusu bao kwa mlinda mlango wa Simba, Aishi Manula, jana rekodi ya michezo dhidi ya Mwadui FC, Yanga na African Lyon ilitibuliwa.
Frank Domayo ambaye amekuwa ni super sub baada ya kuingia akichukua nafasi ya Joseph Mahundi alizima ndoto za Manula kuendelea ubabe wake wa kukaa langoni bila kufungwa.
Dakika ya 81 baada ya mshambuliaji Donald Ngoma kumzungusha anavyopenda Paul Bukaba aliachia pasi murua iliyotua miguuni mwa Domayo bila ajizi aliachia shuti kali.
Shuti hilo ambalo lilimshangaza Manula na mashabiki wa Simba liligonga kwenye mstari wa goli likarejea ndani ya uwanja baada ya kugonga mwamba likakutana na Obrey Chirwa ambaye kichwa cheke kilipaa mawinguni.
Manula anafungwa baada ya kuchza mechi tatu mfuluizo bila kufungwa ambazo ni sawa na dakika 280.
0 Comments