Windows

Manchester United yaichapa Chelsea Darajani

Manchester United yaichapa Chelsea Darajani
Manchester United imefanikiwa kutinga hatua ya Robo Fainali baada ya kuifunga Chelsea bao 2 kwa 0 katika mchezo wa 16 bora ulichezwa katika uwanja wa Stanford Bridge mjini London.
Katika mchezo huo Magoli ya Manchester United yalifungwa na Ander Herera dakika ya 31 akipokea pasi safi kutoka kwa Paul Pogba na Goli la Pili likifungwa na Paul Pogba kwa Kichwa dakika ya 45.
Kipindi cha Pili licha ya mashambulizi ya hapa na pale lakini Chelsea ilishindwa kuchomoa mabao hayo na kuwafanya kutupwa nje ya mashindano hayo ya FA cup.

Post a Comment

0 Comments