Ujio wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Magufuli leo, umeufunika kwa muda Mkutano Mkuu wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) utakaofanyika kesho hapa Arusha.
Rais Magufuli akiambatana na wakuu wa nchi zinazounda Umoja wa Afrika Mashariki, watakutana jijini hapa kwenye mkutano wa 20 wa Jumuiya ambao ni hitimisho la vikao vya maofisa, makatibu wakuu na mawaziri wa wizara mbalimbali kutoka nchi zinazounda jumuiya hiyo ambavyo vilianza Januari 28.
Kuanzia juzi Alhamisi, hali ya usalama jijini Arusha imeonekana kuimarishwa ambapo Askari Polisi wamekuwa wakizunguka mitaani kuhakikisha kunakuwa na utulivu na amani kwenye kipindi hili.
Polisi hao wamekuwa wakifanya doria katika mitaa mbalimbali jijini Arusha na ulinzi huo uneongezeka zaidi asubuhi ya leo Ijumaa ambapo askari waliovaa sare na wale walio na nguo za kiraia wamekuwa wakizunguka huku na kule kuhakikisha kila kitu kinakwenda sawa.
Kwenye Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha AICC ambako ndiko Mkutano wa TFF utafanyika, ulinzi umekuwa ni mkubwa zaidi na kumekuwa na zuio la mtu wa kawaida kusogea eneo hilo.
Ikumbukwe kuwa moja ya kumbi zilizopo katika kituo hicho ndicho kutafanyika Mkutano Mkuu huo wa TFF.
Hali hiyo imelazimisha maofisa wa TFF kuhamishia shughuli mbalimbali za maandalizi ya mkutano huo, kwenye Hoteli ya Palace iliyopo pembeni mwa kituo cha AICC.

0 Comments