Windows

HIZI ZILIKUWA DAKIKA 450 CHUNGU KWA PLUIJM ALIPOKUWA AZAM FC


ALIYEKUWA Kocha Mkuu wa Azam FC, Hans Pluijm kabla ya kupigwa chini kichwa chake kiliwaka moto kutokana na kutumia dakika 450 ambazo ni sawa na mechi tano kuambulia kichapo na sare tu.

Michezo hiyo ambayo Pluijm kwake ilikuwa ni pasua kichwa ni kuanzia ule dhidi ya Alliance ambapo alilazimisha sare ya kufungana bao 1-1 na Alliance, akatoa sare na Lipuli kabla ya kufungwa na Tanzania Prisons kisha sare nyingine mbele ya Coastal Union na kuambulia kichapo cha mabao 3-1 mbele ya Simba kilichowafanya mabosi wamfungie vioo.

Kwenye mechi zote tano mfululizo safu ya ushambuliaji ya Azam inayoongozwa na Obrey Chirwa ilifunga mabao manne na kuruhusu kufungwa mabao 7.

Pluijm  alisema wachezaji walikuwa wanashindwa kupata matokeo kutokana na kushindwa kujiamini, ila kwa sasa baada ya kusitishiwa mkataba anafikiria kurejea Ghana.

Pluijm ameiongoza Azam FC kuwa nafasi ya pili kwenye michezo 25 ameshinda michezo 14 sare 8 na alipoteza michezo mitatu alikusanya pointi 50.

Post a Comment

0 Comments