Windows

KLOPP MTATAT KINOMA, AWATAJA MAJERUHI WA MANCHESTER UNITED KUHUSIKA NA SARE YAKE


Jurgen Klopp Meneja wa Liverpool amesema kikosi chake kiliponzwa na majeruhi ya wachezaji wa timu ya Manchester United hali iliyofanya washindwe kupata matokeo chanya siku ya jana Uwanja wa Old Trafford.
Ole Gunnar Solskjaer alilazimika kufanya mabadiliko kwa wachezaji wake kama Ander Herrera, Jesse Lingard na Juan Mata kabla ya kpindi cha kwanza kuisha.

Kwa hali hiyo Klopp anafikiria mabadiliko hayo yaliua morali ya timu yake kupambana ndani ya uwanja  kupata matokeo.
Alipoulizwa kuhusu kuacha pointi mbili ugenini kwake ni funzo ama ni maumivu alisema " Yote kwa yote ni sawa, hili ni la kawaida kwa kuwa tungepata pointi zaidi ingekuwa vizuri.
"Nilifikiria kabla ya mchezo, namna muundo wa United ulivyo, watu weng wangefikiria juu ya uwezo wetu wa kuisimamisha United hasa tulipokabiliana nao.
"Tulianza mchezo kwa umakini na uhakika ndivyo ambavyo nilitaka tufanye, ilikuwa ni mbinu ya moja kwa moja na tulicheza mira tukapiga pasi huku tukimiliki mpira, ulikuwa mchezo mzuri kwetu ndipo baadaye majetuhi wakafuatia na majanga kwetu kuanza
"Hapo ndio timu yangu ilishindwa kuonyesha maajabu kiukweli sikutaka itokee hali ya namna hiyo na kama utaniambia nieleze ilikuwaje siwezi kueleza kwa uhakika kuhusu jambo hili ila ndivyo iivyokuwa wachezaji walishindwa kumudu hali yao waliyanza nao bali walipunguza ile kasi," amesema.

Post a Comment

0 Comments