

Kocha huyo hadi sasa ameiongoza Yanga kukaa kileleni mwa msimamo wa Ligi Kuu Bara ikiwa na pointi 58 baada ya kucheza michezo 23.
Kocha huyo Jumamosi hii ataiongoza Yanga kwenye ‘Kariakoo Derby’ kupambana na wapinzani wao wa jadi, Simba kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar.
Zahera amesema mechi zao za awamu hii zinakuwa ngumu kutokana na wapinzani wao wengine kuzicheza kwa kutumia timu ambazo wanapambana nazo.
Pamoja na kwamba Zahera hakutaja moja kwa moja lakini hapa anamaanisha kuwa Simba na timu zingine za nafasi za juu zimekuwa zikihujumu mechi zao kwa kuwa ndiyo wapinzani wao wakubwa kwenye ligi.




0 Comments