Windows

HESABU ZA TANZANIA PRISONS MSIMU HUU ZIMEEGEMEA HAPA


KIKOSI cha Tanzania Prisons leo kitakuwa na kazi mbele ya Kagera Sugar kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara ambao ni mzunguko wa pili huku hesabu zao kubwa ikiwa ni kubaki Ligi Kuu Bara.

Prisons msimu huu bado hawajakaa kwenye reli kutokana na kushika nafasi ya 20 kwenye msimamo baada ya kucheza michezo 22 mpaka sasa.

Beki wa Prisons, Salum Kimenya amesema ushindani ni mkubwa kwani kila timu inapania kupata matokeo uwanjani ila wanaamini watakaa sawa kiushindani na kutimiza lengo lao kubaki kwenye ligi.

"Kila timu inapambana kutafuta matokeo nasi pia tunafanya jitihada zetu uwanjani ili kupata matokeo, kikubwa ambacho tunataka kitokee kwa sasa ni kuona tunaweza kubaki kwenye ligi naamini inawezekana, mashabiki watupe sapoti," alisema Kimenya.

Post a Comment

0 Comments