Windows

HAWA HAPA NYOTA WA SIMBA NA YANGA KUIKOSA 'DERBY' KESHO

KESHO Jumamosi, Uwanja wa Taifa Dar es Salaam, Yanga itakuwa mwenyeji wa Simbakatika mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Mchezo wa mzunguko wa kwanza ulimalizika kwa suluhu ya bila kufungana, miongoni mwa wachezaji nyota waliotumikia timu hiyo kesho wanatarajiwa kuukosa mchezo huo kutokana na sababu mbalimbali.

Kwa upande wa Yanga, wachezaji wawili hawatakuwa sehemu ya mchezo nao ni mlinda mlango, Beno Kakolanya ambaye hayupo na timu kwa muda mrefu kutokana na matatizo yake na kocha mkuu, Mwinyi Zahera kugoma kumtumia.

Juma Mahadhi anasumbuliwa na majeruhi hivyo hatakuwa sehemu ya mchezo.

Kwa upande wa Simba ni Shomari Kapombe ambaye ni majeruhi, Shiza Kichuya amejiunga na kikosi cha ENPPI nchini Misri.

Post a Comment

0 Comments