Windows

BODI YA WAKURUGENZI SIMBA YAAMUA, YAELEZWA HAWA NDIYO MAPRO WATAKAOBAKI KIKOSINI MSIMU HUU


Baada ya kikao cha Mwekezaji Mkuu wa klabu ya Simba na Bodi ya Wakurugenzi kumalizika siku chache zilizopita, inaelezwa kuwa kuna uwezekano wa kikosi cha timu ya Simba kupanguliwa.

Taarifa za ndani kutoka Simba zinasema uongozi umedhamiria kufanya usajili wa maana ili kuendana na kasi ya mashindanio ya kimataifa ambayo yanahitaji wachezaji wenye uwezo ansi lelemama.

Sasa, zilizo chini ya kapeti zinasema kuna baadhi ya wachezaji ambao wana uhakika wa kusalia katika kikosi cha kwanza ambao ni wa kimataifa na wengine wakiondoshwa.

Imeelezwa wachezaji Emmanuel Okwi, Meddie Kagere, Clatous Chama na James Kotei ndiyo pekee wa kimataifa walio na uhakika wa kusalia kikosini msimu huu.

Wengine ambao bado wana mikataba na uongozi haujaridhishwa nao wanaweza kuwavunjiwa kisha klabu itafanya usajili mwingine kuendana na matakwa ya mashindano ya kimataifa.

Post a Comment

0 Comments