

OFISA Habari wa Azam FC iliyo chiniya kocha Hans Pluijm, Jafary Maganga amesema ushindani uliopo kwenye Ligi Kuu Bara unafanya matokeo kuwa tofauti na wengi wanavyofikiria.
"Timu nyingi zinafanya vizuri na ushindani mkubwa unaonekana kwenye ligi na wengi wanapokutana na timu bora kama yetu wanaonyesha uwezo mkubwa," amesema.
Azam FC walipata sare mfululizo walianza na Biasahara United Uwanja wa Chamazi kisha wakalazimisha sare mbele ya Lipuli FC na jana walipoteza mbele ya Tanzania Prisons.
Wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 49 na vinara wa ligi ni Yanga baada ya kujikusanyia pointi 58.




0 Comments