Windows

ALIYESHINDA MAMILIONI KUTOKA M-BET AELEZA ATAKAVYOICHANGIA YANGA





Yule Shabiki wa klabu kongwe ya Yanga aliyeshinda fedha zaidi ya Sh milioni 188.5  kutoka M-Bet amesema ataichangia kiasi fulani Yanga.

Shabiki huyo amesema ataichangia Yanga baada ya kurejea kwao mkoani Njombe na kuangalia hesabu zake kwake.


Frank Kayombo mkazi wa Njombe ameibuka mshindi wa milioni 188.5 baada ya kubashiri vyema timu 12 (Perfect 12) ya Kampuni ya Kubashiri ya M-Bet.

“Mimi ni timu ya wananchi hapa nyumbani Tanzania, nje ni Manchester United. Kweli kabisa lazima nitaichangia Yanga lakini acha nitulie kwanza. Baada ya kurejea nyumbani tu nitafanya hivyo, nitaichangia,” alisema akionyesha kujiamini.


Kayombo amekuwa mshindi wa kwanza wa Perfect 12 kwa mwaka 2019 akijinyakulia kiasi hicho cha fedha baada ya mwaka uliopita kupatikana washindi  22. 


Kayombo ameshinda Milioni 188,484,550.

Meneja Masoko wa M-Bet, Allen Mushi amewataka Watanzania waendelee kucheza Perfect 12 huku dau lake likizidi kuongezeka kila mara.


Post a Comment

0 Comments