Windows

ZAHERA ATANGAZA KUCHUKUA MAKOMBE HAYA MATATU LIKIWEMO LA SIMBA


Kocha Mkuu wa Yanga, Minyi Zahera, amefunguka juu ya mataji anayoyahitaji msimu huu wa 2019.

Zahera ambaye amekuwa ndiye mteka habari mkubwa hivi karibuni katika klabu hiyo, ameeleza malengo yake ni kushinda mataji hayo ikiwemo lile la Simba.

Kocha Zahera ameyataja mataji hayo kuwa ni la Ligi Kuu Bara ambalo msimu uliopita lilichukuliwa na Simba.

Aidha, Mkongomani huyo amelitaja Kombe la SportPesa ambalo linatarajia kuanza Januaru 22 ya kesho kulibeba pia ili kujiwekea heshima na lile la FA.

Licha ya Yanga kupitia kipindi kigumu hivi sasa anaamini kuwa kikosi chake kitazidi kuwashangaza wengi 

Post a Comment

0 Comments