LICHA ya Yanga kutolewa hatua ya robo fainali na KK Shark kwa kufungwa mabao 3-2, kocha Mwinyi Zahera ameitaka Simba kupambana kubeba kombe hilo.
Zahera amesema ushindani ni mkubwa na kila timu inahitaji matokeo ila kuna nafasi kubwa kwa Simba kufanikiwa kubeba kombe hilo endapo wataamua.
"Kama sisi tumetolewa bado tuna imani kuna wawakilishi kutoka Tanzania ambao wanaweza kufanya vizuri ikiwa ni pamoja na Simba.
"Naamini wakipambana watabeba kombe ili kuweka heshima kwa ukanda wa Afrika mashariki likiondoka tena nyumbani ni jambo la huzuni kwa mashabiki, sisi tumetolewa kutokana na kushindwa kutumia nafasi tulizotengeneza," alisema Zahera.
Yanga na Singida United ni timu za Tanzania ambazo zilitolewa mapema kwenye hatua ya robo fainali katika mashindano ya SportPesa Cup na kupishana na fuko la hela ambazo ni zawadi zaidi ya milioni 60 anazopewa mshindi wa kwanza.
0 Comments