

Mbunge wa Jimbo la Ilemela Dk. Angeline Mabula ambaye pia ni Naibu Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi ameendeleza mikakati yake kuhakikisha Jimbo lake lina viwanja vya michezo vya kisasa vyenye hadhi ya kimataifa kwa lengo la kuinua na kuendeleza vipaji.
Akizungumza na Waandishi wa Habari katibu wa Mbunge huyo Michael Goyele wakati akikabidhi vifaa vya michezo katika Mtaa wa Buyombe vyenye thamani ya shilingi 320,000/- alisema kuwa Mbunge huyo anapenda michezo kutokana yeye pia mwanamichezo nambari moja kwani anafuatilia pamoja na kudhamini timu mbalimbali zikiwemo za Jimbo Cup na Mbao FC.
TAZAMA FULL VIDEO HAPA CHINI....USISAHAU KUSUBSCRIBE




0 Comments