Msanii wa Filamu nchini, Wastara Juma amesema kuwa amejifunza kitu tangu alipokuwa alipokuwa anaumwa huku akieleza kuwa ni bora anapokuwa na matatizo yake.
Wastara ameiambia, Wasafi Tv kuwa unaweza ukayasema matatizo yako alafu ukaja ukafa kwa presha kwasababu ya kusema tu.
"Lakini Wastara kama Wastara nimejifunza kwamba unapokuwa na matatizo yako bora ufe nayo tu, kwasababu unaweza ukasema alafu ukaumia zaidi kwasababu unaweza ukafa kwasababu ya kusema tu unaweza ukafa kwa presha," amesema Wastara.
Kwenye mitandao ya kijamiii kulikuwa na maneno kuwa Wastara anaomba sana misaada na tapeli huku wengine wakisema anafeki sana maradhi kitu ambacho yeye amekikataa.
0 Comments