Waziri wa Maliasili na Utali, Dkt. Hamisi Kigwangalla amewaita wawekezaji kuja nchini Tanzania kwa ajili ya kuwekeza katika sekta ya Utalii wakati aliposhiriki kongamano la 10 la Uwekezaji na Biashara katika sekta ya Utalii Afrika.
Amebainisha hayo kwenye kongamano lilofanyika jana Madrid nchini Hispania likiwa limeandaliwa na Shirika la Utalii la Umoja wa Mataifa (UNWTO).
“Nawakaribisheni nyote, Njooni Tanzania muwekeze kufuatia uwepo wa mazingira na miundombinu bora kwa ajili uwekezaji katika sekta ya utalii
pamoja na viwanda,” amesema.
Waziri Kigwangalla alipata fursa ya kuwa mmoja wa wazungumzaji ambapo amewahakikishia Wawekezaji wenye nia ya kuja kuwekeza nchini Tanzania kwamba ni sehemu salama ukizingatia hali ya amani na utulivu iliyopo nchini.
0 Comments