Windows

Tutoke kwenye dimbwi hili, kwanini akili hawazitumii - Rais Magufuli


Rais Magufuli ameshangazwa na Benki Kuu ya Tanzania (BoT) kutohifadhi dhahabu ili kuuza kipindi ambacho uchumi umetikisika.

Ameeleza hayo leo kwenye ukumbi wa mikutano wa JNICC jijini Dar es Salaam ambapo ulifanyiwa mkutano mkuu wa kisekta wa Wizara ya Madini.

"Kwanini nchi nyingine zinatunza na dhahabu ili kulinda masoko yao ili dola ikiteremka dhahabu ipo wanaweza wakaiuza, kwanini hizi akili za wataalamu wetu waliopo BOT hawazitumii hapa," amesema Rais Magufuli.

Ameendelea kwa kusema, 'Tunataka tutoke kwenye dimbwi hili la sekta ya madini kuchangia kwa asilimia 4 ifike kwenye kuchangia asilimia 10 au zaidi ya hapo, ili uzalendo wa watanzania uwe umeakisiwa kwenye sekta hii'.



Post a Comment

0 Comments