Mchezaji wa Simba SC, Clatous Chama amesema kuwa wachezaji wa kikosiu hicho wapo tayari kupamba na kutwaa ubingwa wa SportPesa Cup.
Chama amesema furaha ya wachezaji ni kuona wanafuta machozi ya kufungwa mabao 5-0 na AS Vita hivyo watapambana leo mbele ya Bandari kupata ushindi.
"Hesabu zetu ni kuona tunabakiza kombe hili hapa Tanzania msimu huu na lisitoke kwenda nje ya nchi mashabiki waendelee kutupa sapoti tunaweza kufanya makubwa," alisema Chama.
Utakumbuka Chama alifanikiwa kuwa mchezaji bora kwenye mchezo wa robo fainali dhidi ya AFC Leopards na alifunga bao 1 kati ya 2 ambayo walishinda yaliyowapeleka hatua ya nusu fainali.
0 Comments