Windows

Simba SC kupoza machungu ya mashabiki Leo


Uongozi wa Simba umefunguka kuwa utatumia mchezo wao wa leo wa SportPesa Cup utakaochezwa Uwanja wa Taifa kupoza machungu ya mashabiki baada ya kupigwa mabao 5-0 katika mchezo wa Ligi ya Mabingwa nchini Congo.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema anatambua ugumu wa mashindano pamoja na uimara wa wapinzani wao AFC Leopards ila watatumia uzoefu wao kupata matokeo kwenye mchezo wao wa leo.

"Tunajua mashabiki wana maumivu hata sisi pia tunamaumivu ya kupoteza mchezo wetu wa Ligi ya Mabingwa, tutatumia mchezo huu kuonyesha kwamba tunaweza na tutafanya kazi kubwa kutafuta ushindi.

Hata hivyo amesema wapinzani wao pia wanajina la mnyama mkali hivyo leo itakuwa vita watapambana kutafuta matokeo mazuri mashabiki wajitokeze kuona ubora wao.




Post a Comment

0 Comments