Windows

MZEE AKILIMALI AGEUZIA KIBAO SIMBA, AWACHANA KISA KIPIGO CHA VITA, AMSHAURI MANARA JAMBO


Mjumbe wa Baraza la Wazee wa Yanga, Mzee Ibrahim Akilimali, amewachana Simba baada ya kufungwa mabao 5-0 dhidi ya AS Vita katika Ligiya Mabingwa Afrika.

Akilimali amesema ni aibu kubwa kwa timu kama Simba kupata aina hiyo ya matokeo akieleza walisema kuwa wana kikosi chenye thamani ya bilioni 1.3.

Mzee huyo ameongeza kwa kusema ni aibu kubwa na fedha kwa taifa la Tanzania kwani wameitangaza vibaya nchi na hawakustahili kufungwa mabao hayo.

Ameenda mbali zaidi na kumshauri Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara kuwa apunguze maneno zaidi ya kufanya vitendo.

Ameeleza kwamba Manara amekuwa akilemba mambo mengi lakini mwisho wa siku wanaambulia sifuri hivyo ni vema akapunguza kupamba mambo.

Post a Comment

0 Comments