Windows

Mji wa Athens kupata msikiti wake wa kwanza mwezi Machi

Waziri wa elimu na masuala ya dini wa Ugiriki Kostas Gavroglu, ametangaza kwamba kwa mara ya kwanza kutakuwa na msikiti mji mkuu wa Ugiriki Athens.

Msikiti huo ambao ufunguzi wake umeahirishwa mara 5, utafunguliwa mwezi Machi mwaka huu.

Gavroglu, akizungumza bungeni kuhusiana msikiti huo utakaokuwa wa kwanza mjini Athens alisema,

ujenzı wa msikiti huo umekamilika na utafunguliwa ifikapo mwezi Machi mwaka huu.

Msikiti huo utakuwa na ukubwa wa mita za mraba 850, na uwezo wa watu 350.

Msikiti huo hautakuwa na mnara.

Kwa mujıbu wa mipango iliyopo katika msikiti huo kutakuwa na bustani kwa ajili ya watoto.

Baada ya msikiti huo kukamilika litaanzishwa baraza la uongozi la msikiti huo ambalo lıtakuwa na wajumbe 7,  ambao ni kama ifuatavyo 2 ni maafisa kutoka wizara ya mali na elimu, 2 kutoka serikalı ya jiji hilo, 1 kutoka mahakama ya juu na 2 ni wawakilishi kutoka jumuiya ya waislamu.

Mji wa Athens unakadiriwa kuwa na idadi ya waislamu wanaofikia 200. Waislamu hao walikuwa hawana sehemu rasmi kwa ajili ya ibada zao.

from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments