Windows

Maporomoko ya ardhi yasababisha vifo vya watu sita

Maporomoko ya ardhi Kaskazini mwa jiji la Bujumbura nchini Burundi yaliosababishwa na mvua kali yamepelekea  maafa.

Maporomoko hayo yamesababisha nyumba kuporomoka na wakaazi wake kufariki.

Mvua kubwa zilizonyesha usiku katika mji wa Buumbura  zilipekea mmomonyoko wa ardhi na mtelezo wa udongo  katika milima ya Sororezo.

Maporomoko hayo ya ardhi   yameizika nyumba moja iliokuwa na watu 6 na hatimaye kusabisha vifo vya watu hao.

Kwa mujibu wa taarifa za wizara ya ustawi wa jamii ya nchi hiyo mnamo mwaka 2018, familia elfu 60 ziliathiriwa na majanga ya asili.

from MUUNGWANA BLOG

Post a Comment

0 Comments