KOCHA wa Simba, Patrick Aussems amesema kuwa wachezaji wake wamecheza kwa kujituma ila wameshindwa kupata matokeo katika mchezo wa nusu fainali ya SportPesa Cup leo Uwanja wa Taifa kutokana na kushindwa kutumia nafasi walizotengeneza.
Simba leo wametolewa kwenye hatua ya nusu fainali kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Bandari FC ya Kenya na kufanya wasubiri kutafuta mshindi wa tatu.
Aussems amesema wachezaji wake wengi walikuwa wamechoka kutokana na kufanya kazi muda mrefu bila kupumzika hali iliyowafanya washindwe kuonyesha ubora wao katika mchezo wa leo.
"Wachezaji wangu wanacheza sana mpira bila kupata mapumziko kwa muda wa masaa 24 na mechi zote ni za ushindani.
"Bandari ni timu bora ingekuwa ngumu kwangu kupata matokeo kutokana na ubora wa kikosi chao ni muda sasa wa kuangalia namna ya kupanga ratiba ili kuwe na unafuu kwa timu ambazo zinashiriki na kwangu SportPesa Cup ilikuwa ni sehemu ya kuandaa kikosi changu kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Al Ahly," alisema Aussems.
0 Comments