TIMU ya Mbao FC ya Mwanza imefanikiwa kuweka rekodi katika michuano ya SportPesa Cup kufuatia kuwatoa mabingwa watetezi wa michuano hiyo Gor Mahia kwa kuwafunga penalti 4-3 ambao walitwaa kombe hilo mara mbili mfululizo.
Gor Mahia ndiyo timu pekee ambayo imefanikiwa kutwaa ubingwa wa SportPesa tangu ilipoanzishwa mwaka 2017 na kufanikiwa kucheza na timu ya Everton baada ya kupata ubingwa mara mbili.
Aidha, tangu kuanzishwa kwa michuano hiyo, timu za Tanzania hazijawahi kutwaa ubingwa ambapo mwaka jana Simba ilitinga fainali lakini ilitolewa na Gor Mahia, hivyo kuwapa nafasi wapinzani wao hao kusonga mbele.
Hivyo, kutokana na matokeo ya juzi, Mbao ambao ndiyo mara yao ya kwanza kushiriki michuano hiyo, imefanikiwa kujiwekea rekodi ya kipekee kwa kuwatoa mabingwa watetezi ambao walikuwa mwiba kwa timu za Simba na Yanga kwa miaka miwili mfululizo ambayo walishiriki na kuwapa nafasi ya kutwaa ubingwa huo.
Aidha, akizungumzia kutinga hatua ya nusu fainali, Kocha wa Mbao FC, Ally Bushiri ambapo watakutana na Karobangi Sharks, leo alisema:
“Niliandaa kikosi changu vizuri hasa katika suala zima la nidhamu ya mchezo na ndiyo maana tumepata matokeo hayo, kwa sasa natambua nakutana na nani katika hatua ya nusu fainali nitakiandaa kikosi changu kuweza kushinda.”
0 Comments