Windows

Juhudi binafsi zahitajika kunusuru wanafunzi kijiji cha Kinko mkoani Tanga


Kufuatia changamoto ya Umbali wa kusafiri kilomita 7  kwenda na Kurudi ili kupata elimu ya sekondari katika Kijiji  cha Kinko kata ya Lukozi Wilayani Lushoto Mkoani Tanga Wengi wa wanafunzi wanalazimika kukatiza masomo yao kutokana na tatizo hilo.

Akizungumza na Muungwana Blog, Mwenyekiti Msaafu wa Kijiji  cha Kinko kata ya Lukozi Bwana Charles Mavoa amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto hizo pia elimu kwa mtoto wa kike imekuwa tatizo hivyo wengi kulazimika kukatiza masomo yao na kutoroka kusikojulikana na kwenda kufanya kazi mjini.

Amesema kuwa Shule ya Msingi ipo na watoto wanakwenda shule lakini upatikanaji wa elimu ya sekondari bado ni tatizo sugu kutokana na wengi kusafiri umbali wa kilomita zaidi ya 6 kwenda kufuata elimu hiyo ya kidato cha kwanza.

Ameongeza kuwa baadhi ya wanafunzi wengi wamekatiza masomo yao ikiwemo watoto kuolewa na umri mdogo na baadhi ya wazazi kukosa kutambua umuhimu wa elimu kwa mtoto wa kike.

Pamoja na hayo katika kijiji cha Kinko baadhi ya wazazazi hawaoni elimu ni kipao mbele kwao kutokana na mazingira magumu ya upatikanaji wa elimu na ukosefu wa waalimu wa kutosha katika shule ya Msingi Kinko ambayo kwasasa hata majengio yaliopo hayaakisi ubora wa elimu unaotolewa.

Amesisitiza kuwa Elimu ya Mtoto wa Kike katika kijiji hicho cha Kinko iko mashakani kutokana na Mabinti wengi kukatiza masomo kutokana na kuogopa kubakwa kuwa kuwa wanakutana na changamoto nyingi njiani wanaposafiri umbali huo wa kilomita zaidi ya Sita Kwenda kutafuta kidato cha Kwanza na Wengine kupata Ujauzito.

Kijiji cha Kinko Kilichopo Pembezoni mwa Wilaya ya Lushoto bado elimu iko nyuma kutokana na mazingira magumu yaliyopo ikiwemo upatikanaji wa Fedha kwa wengi hutegemea misimu ya mavuno ambayo wakati mwingine haifaikiwi hivyo wengi kulalamikia ugumu wa maisha.

Hivi karibuni, Tulimtafuta Mkuu wa Wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, Januari Lugangika amesema kuwa wajiwekea mikakati mbalimbali kwa kushirikiana na wadau ili kuona ni jinsi gani ya kutoa elimu kuhusu umuhimu wa elimu na kuchukulia hatua wale wote wanaokatiza elimu ya mtoto wa kike kwa njia moja ama nyingine

Post a Comment

0 Comments