Na. John Walter, Babati
Kocha wa timu ya Wananchi Fc yenye makao yake Babati mjini Rioba Kanyenye amesema ushirikiano duni kati ya viongozi na wadau ndio kinachoangusha soka katika mkoa wa Manyara.
Kanyenye ambaye ni kocha wa Zamani wa timu ya Usalama Sc ya daraja la pili amesema Manyara ina vijana wenye vipaji ila viongozi ndio chanzo cha kufanya vibaya kwa kushindwa kutoa hamasa kwa viajana kujituma kwenye soka ndio maana timu nyingi za mkoa huo zinazidi kudorora na kushindwa kusonga mbele.
Aidha Kanyenye ameweka wazi mipango ya Wananchi Fc kwamba ni kuhakikisha wanapanda hadi kufika ligi daraja la pili ngazi ya taifa kwa kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Kanyenye ameeleza kuwa Mpaka sasa timu ya Wananchi Fc ambayo inafanya mazoezi katika uwanja wa Kwaraa mjini Babati ipo katika hatua za mwisho kumalizia usajili ili timu hiyo iweze kutambulika kisheria.
Katika hatua nyingine Kanyenye amempongeza Mkuu wa mkoa wa Manyara Alexander Mnyeti kwa kuwakutanisha wafanyabiashara na kukubaliana kujenga vibanda kuzunguka uwanja wa mpira wa Kwaraa jambo litakaloongeza hamasa ya Michezo na kodi katika mkoa wa Manyara kwa kuvuta timu mbalimbali za ligi kuu Tanzania kucheza katika uwanja huo.
0 Comments