Windows

ILE ISHU YA MWASHIUYA KUPIGWA STOP, IKO NAMNA HII....





Waamuzi wa mchezo kati ya JKT Tanzania na Simba uliopigwa katika Uwanja wa Mkwakawani, Tanga, Mbaraka Rashid amepewa onyo kali kutokana na kutokuwa makini huku msaidizi wake, Mashaka Mwandembwa akifungiwa miezi mitatu.


Wakati waamuzi hao wakikumbana na hilo, wachezaji  wa Singida United, Geofrey Mwashiuya na Rajabu Zahiri wamefungiwa  mechi tatu kila mmoja.


Adhabu hizo na mashauri mengine yamefanywa baada ya Kamati ya Uendeshaji ya Ligi kupitia malalamiko na matukio tofauti ambayo yalitokea katika mechi tofauti za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na Ligi Daraja la Pili, hivi karibuni.

 Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi, Boniphace Wambura amesema: "JKT walileta malalamiko yao juu ya mchezo wao na Simba.


“Malalamiko yamepitiwa na mwamuzi wa mchezo ule Mbaraka Rashid amepewa onyo kali kutokana na kutokuwa makini lakini msaidizi wake Mashaka Mwandembwa amefungiwa miezi mitatu kutokana kushindwa kutafsiri sheria ya kuotea 'offside'.


"Wachezaji wa Singida United, Geofrey Mwashiuya amefungiwa mechi tatu baada ya kumpiga mchezaji wa Biashara United huku Rajab Zahiri katika mchezo huohuo alitaka kumpiga mwamuzi, hivyo kafungiwa mechi tatu na kocha wao Shadrack Nsajigwa amefungiwa mechi mbili na faini ya Sh 500,000 kutokana na kujibizana na mwamuzi.


"Singida wamepigwa faina ya Sh 200,000 baada ya kushindwa kuingia katika vyumba vya kubadilishia nguo na kwenda chumba cha waandishi wa habari walipocheza na Simba. Pia mtunza vifaa wa Ruvu Shooting, Augustine Kalangwa, amepelekwa katika Kamati ya Nidhamu.


"Mbao FC na Alliance zimepigwa faini Sh 500,000 baada ya kushindwa kuingiza timu za U-20 zilipokutana na Kocha wa Makipa wa Lyon, Juma Bomba amefungiwa mechi mbili na faini ya Sh 500,000 baada ya kumjibu vibaya mwamuzi.


"Kocha wa Kitayosce, Hamad Haule amefungiwa mechi mbili na faini ya Sh 500,000 baada ya kutumia simu akiwa kwenye benchi tukio lilitokea kwenye mechi ya Kitayosce na Kilimanjaro," alisema Wambura.



Chanzo :SALEH JEMBE

Post a Comment

0 Comments