Windows

Hili la korosho, walipwe haraka - Rais Magufuli


Rais John Magufuli amesema kuwa ameshatoa maangizo kwa Waziri wa Kilimo na Biashara kuhakikisha wakulima wa korosho wenye kilo chache wanalipwa fedha zao.

Amebainisha hayo mbele ya viongozi wa dini ambapo amekutana nao leo Ikulu Dar es Salaam
walipokutakana kujadili kuhusu maendeleo na changamoto za nchi.

"Hili la korosho bahati nzuri juzi kwenye kikao cha Baraza la Mawaziri nimeshatoa maagizo hawa
wenye korosho chache na wakulima wadogo wasicheleweshewe walipwe haraka na pasiwepo na urasimu," amesema.

Aliendelea kwa kusema, 'Wasikae kuchelewesha watu kulipwa wakati fedha zipo, sasa narudia haya maagizo najua wananisikia, Waziri Mkuu ananisikia nataka wakulima wa korosho walipwe na fedha zipo,'.

Post a Comment

0 Comments