Windows

HAWA HAPA WACHEZAJI WA SIMBA WATAIBEBA TIMU YAO, KOCHA WA CONGO AWAPA MBINU




MABINGWA watetezi Simba leo wanaingia kazini kumenyana na AS Vita ikiwa ni mchezo wa Ligi ya Mabingwa utakaochezwa nchini Congo katika Uwanja wa Mertyrs.

Kocha Mkuu wa Yanga, Mwinyi Zahera ambaye pia ni kocha msaidizi wa timu ya Taifa ya Congo akiwa chini ya Kocha Mkuu wa AS Vita, Frolente Ibenge amesema mashine za kazi za Simba zina uwezo wa kuibuka na ushindi kwenye mchezo wao wakiamua.

"Simba ni timu bora na kama watacheza kwa mtindo ambao walifanya dhidi ya JS Saoura kwa kushambulia na kulinda ni rahisi kupata matokeo ila kama watakuwa na hesabu za kulinda pekee itawagharimu kutokana na spidi ya wapinzani wao kufika langoni.

"Emmanuel Okwi, Meddie Kagere na Claytous Chama wana kazi ya kuisaidia timu kupata ushindi wa mapema hali itakayowapa nguvu ya kupambana katika mchezo wao," alisema Zahera.


Chanzo :SALEH JEMBE

Post a Comment

0 Comments