Windows

Harmonize awaweka roho juu mashabiki wake, kisa?


Msanii wa Bongo Fleva, Harmonize ameweka wazi kuwa siku si nyingi atatagaza ndoto yake kubwa aliyopanga kuitimiza kwa mwaka huu.

Muimbaji huyo kutokea WCB amechapisha picha ya uwanja wa taifa kwenye ukurasa wake wa mtandao wa Instagram na kuelezea yupo mbioni kutangaza ndoto hiyo.

"Ndoto yanga mwaka 2019 mwenzi wa nne, tarehe itatangazwa rasmi, kama unaamini hili linawekana basi tuseme ameni," ameeleza Harmonize.

Bado haijajulikana iwapo Harmonize ana mpango wa kuandaa show hadi kujaza uwanja wa Taifa. Msanii wa Afrika Kusini, Cassper Nyovest amewahi kufanya hivyo mara kadhaa nchini kwao. 



Post a Comment

0 Comments