Mabingwa wa soka Tanzania, Simba wameshusha kifaa kingine, safarii ni mchezaji raia wa Namibia.
Imeelezwa ni mshambuliaji na jina lake halisi ni Sadney Urikhob na amewahi kucheza soka kwao Namibia na Afrika Kusini.
Pamoja na Afrika, Urikhob amekipiga barani Asia katika nchi za Indonesia, Malaysia na Vietnam.
Tayari yuko jijini Dar es Salaam na ameishaonana na kocha Patrick Aussems.
Simba inaonekana inataka kuimarisha safu yake ya ushambulizi kwa sababu ya michuano ya Ligi ya Mabingwa Afrika.
Tayari wachezaji wawili kutoka Ghana na Togo wako Dar es Salaam na jana wameichezea Simba dhidi ya AFC Leopards katika michuano ya SportPesa Super Cup.
TAARIFA ZINAELEZA GAZETI LA SPOTI EXTRA LILILO MTAANI LEO ALHAMISI LIMENASA KILA KITU KUHUSIANA NA UJIO WAKE NA TIMU ALIZOKUWA AKIZICHEZEA.
0 Comments