Windows

ESMA: KUACHWA HAKUJAMFANYA ASHINDWE MAISHA

HAJACHINA! Esma Khan ambaye ni dada wa mwanamuziki wa Bongo Fleva, Nasibu Abdul ‘Mondi’ ameweka wazi kuwa kuachika kwake kwenye ndoa hakujamfanya kushindwa maisha.



Akizungumza na Gazeti la Ijumaa, Esma ambaye ni mama wa watoto wawili alisema kuna wanawawake wengine wakiachwa huwa wanakuwa kama wamepatwa na ugonjwa wa kuwafanya washindwe kufanya chochote maishani wakiwaza tu mapenzi, jambo ambalo halipaswi kufanywa na mwanamke anayejitambua.



“Ukweli ni kwamba kuachika kwangu hakujanifanya nishindwe kuendelea na maisha yangu ya kujitafutia riziki. Kwanza nilipoachwa ndiyo maisha yakaninyookea,” alisema Esma ambaye aliolewa na meneja wa wasanii wa Bongo Fleva, Hamad Manungwi ‘Petit Man’ kabla ya kutengana mwaka jana.

Post a Comment

0 Comments