Windows

China awalaumu Yondani, Dante




KIUNGO wa zamani wa Yanga Athumani China amewatipia lawama mabeki na kipa wa timu yake hiyo zamani kwa kuruhusu bao kwenye mchezo wa Ligi Kuu dhidi ya Stand United.

Yanga ilipoteza mchezo wake wa kwanza wa Ligi Kuu ya Soka ya Tanzania Bara kwa kufungwa bao 1-0 na Stand United na kuhitimisha safari ndefu ya timu hiyo kutokupoteza mechi kwenye ligi hiyo.

China aliyewahi pia kutamba na Simba kwenye miaka ya 1990 alitazama goli hilo kupitia video na kuwatupia lawama mabeki Kelvin Yondani, Andrew Vicent’Dante’ na kipa Claus Kindoki.

“Wote wanastahili lawama, huyu beki wa pembeni(Yondani) kwa kuruhusu krosi kwani alikuwa na muda mwingi wa kumsogolea yule wingi kisha akazuia krosi. Lakini kipa nae(Kindoki) na mabeki wa kati(Dante na Gadiel) walitakiwa kujiandaa na tukio lolote ikiwa krosi imepigwa na hawakufanya hivyo.

“Ndio mpira wa kitanzania mapungufu yapo lakini hatujifunzi kile tunachotazama kwenye televisheni. Kitu cha kwanza kwa mchezaji yoyote aliyepo nafasi ya pembeni ni lazima afanye kila afanyalo kutoruhusu krosi kuingia golini kwenu kwani unakuwa haujui wenzako wamejipangaje, kwani krosi ni nusu goli,”alisema.

China baada ya kuangalia kipande hicho cha video. Hata hivyo nyota huyo wa zamani wa kimataifa wa Tanzania alisema kuwa bado timu yake hiyo ya zamani ina nafasi ya kushinda taji la Ligi Kuu msimu huu kama hawataruhusu makosa kama hayo yajirudie.








Post a Comment

0 Comments