KIUNGO wa Simba, Clatous Chama amesema kwake kuchukua tuzo ya mchezaji bora wa mechi katika mashindano ya SportPesa si kitu muhimu sana kama kutinga nusu fainali ya mashindano hayo.
Chama ‘Triple C’ anaamini wataifunga Bandari FC ya Kenya leo
Ijumaa na kutinga fainali ya mashindano hayo ikiwemo kutwaa ubingwa.
Mchezaji huyo alionyesha kiwango kikubwa katika mchezo huo na kuibuka mchezaji bora hivyo kukabidhiwa dola 500 sawa na sh 1.2 milioni za Tanzania.
“Nafurahi kufunga katika mchezo huo na pia kuibuka mfungaji bora ingawa kutinga nusu fainali ni muhimu zaidi kwetu.“Nawashukuru wachezaji wenzangu ambao tumekuwa tukishirikiana kuhakikisha tunaipa timu matokeo mazuri.
“Tumetinga nusu fainali na tutajituma kuweza kufika fainali na
hatimaye kutwaa ubingwa ili uwe zawadi kwa mashabiki wetu ambao hawachoki kutusapoti na kila mara wamekuwa wakituunga mkono,”alisema Chama.
Chama alionyesha kiwango kizuri katika mchezo huo akishirikiana vema na mshambuliaji Emmanuel Okwi ambaye alifunga bao la kwanza.
Simba iliifunga AFC Leopards mabao 2-1 na leo itaikabili Bandari FC inayonolewa na mshambuliaji wa zamani wa Yanga Benard Mwalala.

0 Comments