Windows

ALIYEACHIWA NA CHELSEA KUANZA NA REAL MADRID


ALVARO Morata, ambaye amejiunga na Atletico Madrid kwa mkopo, ataanza kuonyesha cheche zake dhidi ya timu yake ya zamani, Real Madrid.

Atletico itavaana na wapinzani wao wa jadi, Real Madrid kwenye mechi ya La Liga itakayopigwa Februari 9, kwenye Uwanja wa Wanda Metropolitano.

Ni wazi kuwa jambo hilo litampa presha kubwa Morata kwani alikulia Real Madrid ambao ndio wamemsaidia kumpa jina lakini sasa atavaana nao akiwa na wabaya wao, Atletico Madrid. Morata, ambaye inadaiwa ana mapenzi ya tangu utotoni na Atletico, bila shaka atapata wakati mgumu kutoka kwa mashabiki wa Real Madrid, ambao watamwona kama msaliti.

Morata, ambaye amejiunga na Atletico akitokea Chelsea, alipoulizwa kama atashangilia kama akifunga, aligoma kujibu swali hilo. Aliwahi kuchezea kwa mkopo, Juventus hatakuwemo kwenye kikosi kitakachoivaa Real Betis, Jumapili ijayo. Morata sasa ana nafasi ya kuonyesha makali yake baada ya kuwa na wakati mgumu katika kikosi cha Chelsea

Post a Comment

0 Comments