Windows

Wakala avuruga usajili wa Kotei Yanga




Wakala wa kiungo James Kotei raia wa Ghana ameigomea klabu ya Kaizer Chiefs kumtoa kwa mkopo mteja wake kwenda klabu ya Yanga

Uongozi wa Yanga kwa kushirikiana na wadhamini wao GSM walifikia makubaliano na Kaizer Chiefs kumchukua nyota huyo kwa mkopo

Yanga ilikuwa tayari kumchukua Kotei kwa mkataba wa mkopo wa miezi sita. Ingemlipa mshahara wake pamoja na stahiki nyingine kulingana na mkataba

Hata hivyo imebainika Wakala wake ameweka ngumu akiitaka Kaizer Chiefs ivunje mkataba wake kama hawamuhitaji

Lakini pia inaelezwa kuwa Kotei mwenyewe ameweka kipaumbele kurudi kwao Ghana kuungana na familia yake ambapo mkewe amejifungua hivi karibuni

Pia nyota huyo anahofia kujiunga na Yanga kuwa ataharibu mahusiano yake mazuri na mashabiki wa Simba ambao anadai kuwa anawaheshimu

Post a Comment

0 Comments