Windows

Mtaalam wa viungo atua Yanga




Wadhamini wa Yanga GSM wameendelea kulisuka benchi la ufundi baada ya kumshusha kocha wa viungo Riedoh Berdien ambaye pia atakuwa kocha msaidizi wa pili

Berdien ametua nchini akiwa ni pendekezo la kocha mkuu Luc Eymael aliyewasili mapema wiki hii

Berdien raia wa Afrika Kusini anatajwa kuwa mmoja wa wataalam bora kabisa kwenye eneo la kutunza utimamu wa kimwili wa wachezaji



Ana uzoefu wa zaidi ya miaka 12, amefanya kazi katika mataifa sita tofauti barani Afrika

Karibuni alikuwa kocha wa viungo wa timu ya Taifa ya Wanawake ya Afrika Kusini maarufu kama Banyana banyana

Wakati kocha Micho akitoka Orlando Pirates na kujiunga na Zamaleki alimpendekeza kuungana nae nchini Misri

Hata hivyo Berdien hakuwa tayari kufanya kazi nchini Misri

Mafanikio yake ni kushiriki kombe la dunia la Wanawake akiwa na Banyana Banyana mwaka 2019

Pia mwaka 2018 alitwaa taji la Nedbank akiwa na Free State Stars iliyokuwa ikinolewa na Luc Eymael

Mwaka 2017 akiwa na timu ya Taifa ya Togo, walifuzu fainali za AFCON 2017

Lakini pia ameshinda medali tatu za dhahabu kwenye michuano ya COSAFA akiwa na Banyana Banyana

Hakika Yanga imepata mtaalam kwelikweli ambaye anafahamika ndani na nje ya Afrika Kusini

Post a Comment

0 Comments