Windows

Uongozi simba watoa tathimini ya mchezo wao na yanga

UONGOZI wa Klabu ya Simba umewaambia wanachama wake kuwa mahudhurio ya mechi dhidi ya watani wao wa jadi Yanga uliochezwa Januari 4 mwaka huu yalikuwa na zaidi ya watazamaji 57000 waliokuwepo uwanjani wakati wa mchezo huo.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa leo Januari 9,2020 ,Uongozi wa Klabu ya Simba umeelezea mambo mbalimbali kuhusu mechi yao dhidi ya Yanga ambapo umesema mahudhurio katika mechi hiyo iliyochezwa Januari 4 mwaka huu  yanatia moyo kuona Uwanja wa Taifa ukijaa kwa namna ile huku mashabiki wa Simba wakizajaza zaidi ya asilimia 70 ya mahudhurio,

"Tunawapongeza washanguliaji wetu kwa kujaza Uwanja na kwa kushangalia timu yetu katika mchezo uliokuwa na jumla ya magoli manne ,tumeendelea kutangaza chapa yetu,wadhamini wetu Sports Pesa ambao ni wadhamin wakuu, MO Halisi,MO Extra,UHLSPORT na Azam TV. Wanaona thamani ya kudhamini na kujihusisha na chapa yetu ya Simba,"umesema uongozi wa Simba.

Umesema katika kipindi chote cha maandalizi na baada ya mechi wameendelea kupokea maoni kupitia kurasa zao za mitandao ya kijamii ,hivyo itapendeza kuona jinsi klabu ilivyokuwa karibu na mashabiki wake. " Jumla ya makusanyo ya mechi yalikuwa ni Sh.539, 120,000 na haya ni matokeo ya mikakati ya kuwapa thamani mashabiki wetu  na kukuza mapato ya klabu ya Simba,chapa yetu inazidi kukua na tunafurahishwa na maendeleo haya,"umesema.

Pia matarajio waliyonayo kwa timu yalikuwa ni makubwa sana,hata hivyo ambayo wameyapata sio yale ambayo yalitarajiwa na mashabiki wa Simna hawategemei kitu kingine zaidi ya ushindi dhidi ya wapinzani wao wa jadi.Hata hivyo hakuna budi kupokea alama moja iliyopatikana na kusonga mbele.

"Kumekuwa na mengi ya kujifunza kutokana na mechi hii,benchi la ufundi likiongozwa na Kocha Mkuu Svenen Van  den Broeck litaendelea kuyafanyia kazi mapungufu yote yaliyojitokeza,"umesisitiza

Wakati huo huo uongozi huo umesema ukiwa umeridhishwa  na mapato pamoja na ukuaji wa chapa ya Simba kwenye mechi ya watani wa jadi ,wameguswa na kauli zilizotolewa kabla ya mechi hiyo na viongozi wenzao wa timu ya Yanga ,hivyo wanakemea kauli hizo zisizo na tija na zenye lengo la kuiharibu taaswira na heshima ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania(TFF).Tunachukua hatua ya kufikisha malalamiko yao dhidi ya kauli hizo mbele ya Bodi ya Ligi na kwa TFF,"umesema.

Pia wanaendelea kuwa bora na kuipeleka timu yao kwenye nyanja za kimataifa na wanaomba mashabiki wao wote  kuendelea kuishangilia na kuipenda chapa yao  na kuendelea kujaza Uwanja.

"Mwenyekiti wa Bodi anapenda kuwakumbusha kuwa chachu ya kutafuta mafanikio zaidi ndio dira ya Simba ,tukiwa kwenye mashindano  ya Kombe la Mapinduzi 2020 Zanzibar. Tunaendeleza umakini kwa kuboresha timu yetu na kuhakikisha tunapata matokeo mazuri.

Post a Comment

0 Comments