Windows

Kanda aanza mazoezi mepesi



Winga wa timu ya Simba, Deo Kanda ameanza mazoezi mepesi na muda si mrefu ataonekana uwanjani, baada ya kuumia katika mchezo wa Ligi Kuu Tanzania Bara dhidi ya Yanga.

Kanda alipata jeraha la kifundo cha mguu katika mchezo huo, uliochezwa Januari 4, mwaka huu, kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam na kumalizika kwa sare ya mabao 2-2.

Mcongomani huyo anatarajiwa kuungana na wenzake wiki hii, alibaki jijini Dar es salaam wakati wenzake wakielekea Zanzibar kushiriki michuano ya kombe la Mapinduzi



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments