Wanayanga wana kila sababu ya kutamba na kutembeakifua mbele kwani kwa hakika yajayo yanafurahisha
Jana baada ya kuwapa mikataba ya miezi 18 Kocha Mkuu Luc Eymael na kocha wa viungo Riedoh Berdien ambaye pia anakuwa kocha msaidizi namba mbili, aliyekuwa Kaimu Kocha Mkuu Charles Mkwasa amejumuishwa kwenye benchi la ufundi
Mkwasa ndiye kocha msaidizi namba moja ambaye atashirikiana na Eymael na Riedoh
Uongozi wa Yanga umechukua uamuzi sahihi wa kumbakisha Mkwasa kwenye benchi la ufundi kwani tangu akabidhiwe mikoba iliyoachwa na Mwinyi Zahera, alifanya vizuri
Mkwasa ana uzoefu mkubwa wa soka la Tanzania, lakini pia anawafahamu vyema wachezaji wa kitanzania
Atakuwa msaada mkubwa kwa Mbelgiji Eymael ambaye ana watani nzuri ya kushinda mataji katika timu alizofanya kazi
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments