Yanga Princess leo imeshindwa kutamba mbele ya watani zao Simba Queens baada ya kukubali kipigo cha mabao 3-1 katika mchezo wa ligi kuu ya Wanawake ambao umepigwa uwanja wa Karume
Simba Queens ilitangulia kufunga bao la kuongoza kupitia kwa Mwanahamisi Omary kabla Shelda Boniface hajairudisha Yanga Princess mchezoni kwa bao safi dakika ya 25
Hata hivyo mabao mawili ya Mwanadada Neema Kilinga yalivuruga matumaini ya Yanga Princess kutoka angalau na alama moja kwenye mchezo huo
Pamoja na kipigo hicho, kikosi cha Yanga Princess kimeonyesha kuimarika ukilinganisha na timu ya msimu uliopita
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store
0 Comments