Uongozi wa Yanga umepanga kumpeleka beki Lamine Moro Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF) kama watathibitisha kuwa barua zinazosambaa kwenye mitandao ya kijamii ameziandika yeye
Lamine inaelezwa amesharejea kwao nchini Ghana baada ya kuchukua uamuzi wa kuvunja mkataba na Yanga, barua yake ya kuvunja mkataba ilisambazwa kwenye mitandao ya kijamii juzi
Katibu Mkuu wa Yanga Dk David Luhago amesema masuala ya mikataba hayajadiliwi kwenye mitandao ya kijamii kwani ni makubaliano binafsi baina ya pande mbili
Kama itabainika barua hizo aliziandika yeye, uongozi wa Yanga umesema tukio hilo ni sawa na uchonganishi hivyo watamchukulia hatua
Katika hatua nyingine uongozi wa Yanga umesisitiza kuwa mishahara wanayodaiwa na wachezaji si zaidi ya miezi miwili
Hivyo barua hiyo inayosambaa ambayo inadaiwa kuandikwa na Moro, anadai kuwa hakulipwa mshahara miezi mitatu, watahitaji kupata uthibitisho wa madai hayo
Ahusishwa na Simba
Zipo taarifa kuwa Lamine ameshasaini mkataba wa awali kuitumikia klabu ya Simba
Pamoja na kuwa bado hakuna uthibitisho , ukweli utafahamika baada ya usajili wa dirisha dogo kufunguliwa wiki ijayo
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments