Mwili wa nyota wa zamani wa kimataifa wa Yanga na Taifa Stars, Ally Yusuf 'Tigana' aliyefariki dunia jana mchana, umezikwa leo kwenye makaburi ya Msasani, jijini Dar es Salaam.
Wananchi, wadau mbalimbali wa soka nchini wamejitokeza kwa wingi kumpumzisha nyota huyo aliyetamba miaka ya 90 na mwanzoni mwa miaka ya 2000
Tigana alizichezea klabu mbalimbali ndani na nje ya nchi zikiwamo Pan Africans, Yanga, Simba na Cadets ya Mauritius alikumbwa na mauti katika hospitali ya Amana baada ya kuugua ghafla alipoenda kumtembelea mkewe aliyelazwa hospitalini hapo
Hali yake ilibadilika zaidi aliporejea nyumbani na kuwahishwa Hospitalini hapo akilalamika tumbo linamsumbua
Mwenye ez Mungu ampe kauli thabit na amuepushe na adhabu za kaburi
AMEN
Kwa habari zaidi Download App ya soka kiganjani kutoka Play Store.
0 Comments