Beki wa kulia wa Yanga Paulo Godfrey 'Boxer' amekanusha taarifa zinazosambazwa kwenye mitandao ya kijamii kuwa matibabu duni anayopatiwa na uongozi wa Yanga ni chanzo cha yeye kuwa nje kwa muda mrefu
Boxer ambaye leo ameanza mazoezi mepesi, amesema amekuwa akipatiwa tiba nzuri na matarajio yake atarudi uwanja siku sio nyingi
"Namshukuru Mwenye ez Mungu sasa ivi naendelea vizuri na matibabu na nimeshaanza mazoezi mepesi. Natibiwa kwenye Hospitali ya Dk Maliali. Sasa ivi niko vizuri na mazoezi nimeshaanza," amesema
"Niwajulishe wadau wa soka na mashabiki wa Yanga kuwa mimi sitibiwi Manzese kama watu wanavyoongea, natibiwa kwa Dk Maliali, niko vizuri siku sio nyingi nitarudi uwanjani"
Boxer aliumia kwenye mchezo wa ligi ya mabingwa dhidi ya Township Rollers ambao ulipigwa August 10 kwenye uwanja wa Taifa
Alitonesha majeraha hayo ya nyama za paja katika mchezo wa marudiano uliopigwa nchini Botswana August 24
Tangu wakati huo Boxer amekuwa akipatiwa matibabu na mara kadhaa amejaribu kurejea dimbani bila ya mafanikio
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments