Zimebaki takribani wiki tatu na ushee kupigwa kipute cha kwanza cha mchezo wa watani wa jadi kati ya Simba dhidi ya Yanga
Mchezo huo utapigwa January 04 2020 kwenye uwanja wa Taifa, Simba ikitarajiwa kuwa mwenyeji
Mkongwe mwenye historia yake Abdallah Kibaden 'King' amesema anatamani kuona rekodi ya kufunga mabao matatu 'hat-trik'ikivunjwa kwenye mchezo huo
Kibaden ndiye mchezaji pekee aliyefunga mabao matatu kwenye mchezo wa watani wa jadi, mwaka 1976 akiingoza Simba kuibuka na ushindi wa mabao 6-0 dhidi ya Yanga
Baada ya utambulisho wa Mo Simba Arena huko Bunju, Kibadeni amesema furaha ya Wanamsimbazi itatimia zaidi kwa ushindi mnono dhidi ya Yanga January 04
"Ni kitu kikubwa kimefanyika, haijawahi tokea kwa miaka yote, nawaomba wachezaji ili kurudisha fadhila ni kufanya vizuri, tena nataka mechi ijayo na Yanga tushinde, hii itakuwa furaha pekee kwa mwekezaji wetu," amesema
"Mimi nilifunga mabao matatu kwenye moja ya michezo, rekodi ambayo bado haijavunjwa. Nitafurahi kuona Kagere au mchezaji mwingine anafunga mabao matatu siku hiyo"
Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.
0 Comments