

Kabla ya mchezo dhidi ya KMC, kulikuwa na mjadala baada ya uongozi wa Yanga kuamua kutowajumuisha kikosini nyota wake wanne Ally Ally, Mohammed Issa 'Banka', Feisal Salum na Abdulaziz Makame 'Bui' wakiwaruhusu kwenda kujiunga na timu ya Taifa ya Zanzibar
Sababu zilizotolewa na uongozi kuhusu kutojumuishwa kwa wachezaji hao hazikuwa na mashiko kwani muda ulikuwepo, wangeweza kurejeshwa na wakashiriki mchezo dhidi ya KMC
Leo Yanga ilielemewa hasa safu ya kiungo, wachezaji hawakuwa katika kasi iliyozoeleka, walionekana wamechoka pengine ni kutokana na kucheza mechi mfululizo
Pengine uongozi wa Yanga haukuangalia athari ambazo zingeweza kutokea kutokana na ukaribu wa michezo hiyo
Kwani wamecheza na Alliance Ijumaa, wamesafiri kutoka Mwanza, wameendelea na mazoezi bila ya kupumzika na leo wameshuka dimbani
Kwa bahati mbaya kikosi kilichocheza na Alliance ni kile kile kilichoanza dhidi ya KMC leo isipokuwa Sadney
Lakini kama nyota hao wangerejeshwa pengine kocha Charles Mkwasa angekuwa na wigo mpana wa wachezaji wa kuwatumia
Klabu ya Azam Fc jana kwenye mchezo dhidi ya JKT Tanzania, iliwatumia nyota wake walioitwa kujiunga na timu ya Taifa ya Zanzibar na wamewaruhusu leo kurejea Zanzibar
Pengine Yanga nao wangeweza kufanya hivyo



0 Comments