Windows

Ajib kama De Broyne tu



Jana nusu ya mabao yaliyofungwa na Simba kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya Arusha Fc yalipita mguuni kwa Ibrahim Ajib

Katika mchezo huo ambao Simba iliondoka na ushindi wa mabao 6-0, Ajib alitengeneza mabao mawili na mwenyewe kufunga bao moja

Bao la kwanza alimsetia kiungo mkabaji Gerson Fraga huku jingine akimtengenezea Deo Kanda

Bao alilofunga lilitokana na pasi murua iliyopigwa na Clatous Chama

Mambo yanayofanywa na Ajib unaweza kuyafananisha na yale yanayofanywa na kiungo mkali wa Manchester City Kelvin De Bruyne

Ni dhahiri, Ajib aliyejiunga na Simba mwanzoni mwa msimu akitokea klabu ya Yanga, atakuwa mmoja wa wachezaji watakaofurahia ujio wa kocha mpya Sven Vandenbroeck kwani koicha huyo ameonekana kuvutiwa na kiungo huyo mwenye kipaji cha hali ya juu



Kwa habari zaidi Download App ya SOKA KIGANJANI kutoka Play Store.

Post a Comment

0 Comments